26 Februari 2013 - 17:49

Wakenya watakwenda kupiga kura hapo Machi 4 kumchagua kiongozi atakayeiongoza nchi hiyo. Wagombea wa kiti cha urais watafanya mjadala wa pili kujieleza juu ya yale watakayoyafanya pindi wakichaguliwa.

Mjadala wa huu wa sasa utashughulikia masuala makuu ya uchumi na ardhi pamoja na mambo mengine. Kwa kutaka kufahamu zaidi Sekione Kitojo amezungumza na Mwenyekiti wa muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanaojihusisha na ardhi (Kenya Land Alliance) Odenda Lumbumba ambaye kwanza alitaka kujua kwa nini hivi sasa suala la ardhi limepata kipaumbele zaidi.

Makundi ya kuhubiri amani kujitokeza Kenya  

Wakati huu zikihesabiwa siku kabla ya uchaguzi wa Machi 4, makundi mbali mbali ya kijamii yamejitokeza kuhubiri amani kuhakikisha uchaguzi huo wa kihistoria unafanyika bila vurugu yoyote.

Kundi moja la Wakenya mashuhuri linalojiita “Group of Concerned Kenyans Initiative” likiongozwa na Kanali Mstaafu Generali Daniel Opande pamoja na wanachama wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Kenya, Abbas Gullet, limezindua mpango wa kuwashirikisha wanasiasa kuleta amani wakati wa uchaguzi.